Loading
UWAKASEMI ni Umoja wa waliosoma seminari ya Katoke kuanzia mwaka 1964 na umoja huu ulianzishwa mwaka 2021 na kupata usajili rasmi No:BDC/KGR/KIJ.585/WNM/1459 mwaka 2022 kwa mujibu wa sheria
“UWAKASEMI ni umoja wa waliosoma seminari ya Katoke kuanzia mwaka 1964 na umoja huu ulianzishwa mwaka 2021 na kupata usajili rasmi No:BDC/KGR/KIJ.585/WNM/1459 mwaka 2022 kwa mujibu wa sheria.
Kudumisha mshikamano na udugu miongoni mwa wanaumoja waliowahi kusoma Seminari ya Katoke, bila kujali daraja, taaluma au eneo walilopo sasa.
Kuhifadhi na kuendeleza maadili ya Kikristo na msingi wa malezi bora waliyojifunza katika Seminari ya Katoke.
Kuchangia maendeleo ya Seminari ya Katoke kwa hali na mali – ikiwa ni pamoja na miundombinu, vifaa vya elimu, na motisha kwa walimu na wanafunzi.
Kusaidiana katika maisha ya kijamii na kiroho, hasa nyakati za shida au furaha kama vile misiba, harusi, Jubilei, ugonjwa, nk.