U W A K A S E M I

Loading

UWAKASEMI ni Umoja wa Waliosoma Seminari ya Katoke kuanzia Mwaka 1964 na Umoja huu ulianzishwa mwaka 2021 na kupata usajili rasmi No:BDC/KGR/KIJ.585/WNM/1459 mwaka 2022 kwa mujibu wa Sheria

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

Mshikamano

Kudumisha mshikamano na udugu miongoni mwa wanaumoja waliowahi kusoma Seminari ya Katoke, bila kujali daraja, taaluma au eneo walilopo sasa.

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

Maadili

Kuhifadhi na kuendeleza maadili ya Kikristo na msingi wa malezi bora waliyojifunza katika Seminari ya Katoke.

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

Maendeleo

Kuchangia maendeleo ya Seminari ya Katoke kwa hali na mali – ikiwa ni pamoja na miundombinu, vifaa vya elimu, na motisha kwa walimu na wanafunzi.

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

Umoja

Kusaidiana katika maisha ya kijamii na kiroho, hasa nyakati za shida au furaha kama vile misiba, harusi, Jubilei, ugonjwa, nk.

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

Elimu

Kuwezesha wanaumoja kielimu na kiuchumi kupitia mitandao ya wahitimu, semina, warsha, na fursa za uwezeshaji.

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

Hamasa

Kuwahamasisha vijana waliosoma Seminari ya Katoke kuhusu thamani ya elimu na malezi bora kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania.

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

vipaji na taaluma

Kushiriki katika shughuli za kijamii na maendeleo ya taifa, kwa kutumia vipaji, taaluma na uzoefu wa wanachama katika nyanja mbalimbali.

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

Kumbukumbu

Kudumisha mawasiliano na kumbukumbu muhimu kwa kuweka rekodi za wanachama, machapisho, historia ya seminari ya Katoke na mafanikio ya wahitimu.

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

Miradi

Kuendelea kuhamasishana kwa umoja wetu kuwa na miradi ya pamoja ambayo itasaidia kuongeza thamani kwa wanaumoja ambao watakuwa wamechangia .

img
  • Biharamulo, Kagera-Tanzania

Mihadhara

Kushiriki katika Mihadhara mbalimbali inayoitishwa na Umoja wa Waseminari ya Katoke kwa lengo la kusaidia katika kukuza uelewa katika Nyanja mbalimbali kutoka miongoni mwetu.