U W A K A S E M I

Loading

UWAKASEMI ni Umoja wa Waliosoma Seminari ya Katoke kuanzia Mwaka 1964 na Umoja huu ulianzishwa mwaka 2021 na kupata usajili rasmi No:BDC/KGR/KIJ.585/WNM/1459 mwaka 2022 kwa mujibu wa Sheria

kuongeza thamani kwa wanaumoja

Ili kuweza kufikia malengo yaliyotajwa katika malengo makuu
, UWAKASEMI inavyo vyombo mbalimbali vya Maamuzi:

  • Chombo kikuu cha maamuzi cha Umoja.
  • Hujumuisha wanachama wote hai kutoka ndani na nje ya nchi.
  • Huidhinisha bajeti, mipango mikuu, mabadiliko ya katiba, na kuchagua viongozi wa Umoja.
  • Hukutana mara moja kwa mwaka (Annual General Meeting).

    1) Mwenyekiti: majukumu yake ni pamoja na

  • i. Kiongozi mkuu wa Umoja,
  • ii. Msemaji rasmi wa umoja,
  • iii. Kuongoza Mikutano mikuu
  • iv. Mjumbe wa kamati ya Maendeleo

  • 2) Makamu Mwenyekiti

  • i. Huchukua nafasi ya Mwenyekiti anapokosekana.
  • ii. Kusimamia kamati ndogo ndogo atakazo pangiwa na umoja
  • iii. Mjumbe wa kamati ya maadili na nidhamu

  • 3) Katibu Mkuu

  • i. Anasimamia na kuratibu shughuli za kila siku za UWAKASEMI,
  • ii. Kuandaa maandiko na mawasiliano rasmi ya UWAKASEMI
  • iii. Mjumbe Kamati ya Maendeleo ya Seminari ya Katoke

  • 4) Naibu Katibu Mkuu

  • i. Anamsaidia Katibu Mkuu,
  • ii. Hushughulikia kumbukumbu na taarifa.

  • 5) Mweka Hazina

  • i. Anasimamia fedha za Umoja na mali nyingine.
  • ii. Mjumbe wa kamati ya mipango na maendeleo
  • iii. Mjumbe Kamati ya Fedha na Mipango

  • 6) Wajumbe Wakuu

  • i. Wasimamizi wakuu wa kamati za Kitaalamu
  • ii. Wajumbe na washauri wakuu wa kamati kuu


  • i. Kamati ya Maendeleo ya Seminary
  • ii. Kamati ya maadili na nidhamu
  • iii. Kamati ya fedha na Mipango
  • iv. Kamati ya mawasiliano na uanachama.
  • v. Kamati ya UWEKEZAJI ya wana umoja wa UWAKASEMI